- Rais wa Shirikisho la soka Tanzania Wallace Karia amesikitishwa na mijadala inayoendelea kuhusu WAAMUZI.
- Rais Karia amesema, imefika kipindi ushabiki wa Usimba na Uyanga umepelekea kuwatoa mchezoni waamuz, kiasi kwamba baadhi yao wanaogopa hata kuchezesha mechi hizo zinazohusisha Simba na Yanga.
- Ameendelea kusema, makosa mengi yanayotokea uwanjani ligi kuu ni makosa ya KIBINADAMU, waamuzi pia ni binadamu hata kwenye nchi zilizoendelea matatizo hayo yapo ndio maana wakaleta (VAR).
- Licha ya kuleta VAR lakini bado kuna makosa yanatokea amesema Karia.
- Wapo watu wanaamsema tutumie VAR, hizo gharama za VAR tutazitoa wapi ? kwa sababu mchezo mmoja ukitumia VAR inagharimu Tsh 10 Milioni amefafanua Karia.
- Pia amesema suala la kukodi waamuzi nje ya nchi kwa ajili ya Simba na Yanga SC hatuwezi kufanya huo ujinga.
#NBCPremierLeague
0 Comments