seebait header

Andriy Shevchenko, Kocha mpya wa Genoa

 


Mchezaji bora wa zamani Ulimwenguni, Andriy Shevchenko mwenye umri wa miaka 45, raia wa Ukraine ambaye ni fowadi wa zamani wa AC Milan na Chelsea ameingia mkataba wa kuifundisha klabu ya Genoa C.F.C mpaka 2024.


Genoa C.F.C ambao wanashiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A) wameingia mkataba na Andriy ambao utadumu hadi mwaka 2024.

Ujio wake unajaza pengo la Davide Ballardini aliyefutwa kazi na Genoa C.F.C mwezi Novemba 6, 2021.


Shevchenko aliongoza timu ya taifa ya Ukraine kutinga robo fainali za Euro 2020 ambapo walichakazwa na Uingereza 4-0 mjini Roma, Italia. Aidha, alijiuzulu Agosti 2021, wiki chache baada ya mtanange wa Euro 2020 kukamilika rasmi.


Kutua kwake nchini Italia inakuja siku chache baada Wamiliki wapya wa Genoa kutoka Marekani, kampuni ya uwekezaji binafsi ya 777 Partners, kuchukua hatua hiyo haraka huku klabu ikiwa kwenye eneo la kushushwa daraja ikiwa imeshinda mchezo mmoja pekee katika mechi 12 za ligi msimu huu.


Shevchenko anarudi kaskazini mwa Italia miaka 15 baada ya kuondoka AC Milan, ambapo alishinda nayo taji la Serie A, Ligi ya Mabingwa, Coppa Italia, Super Cup ya Italia, na UEFA Super Cup. Raia huyo wa Ukraine pia alitwaa tuzo ya Ballon d'Or 2004 wakati alipokuwa San Siro.


Sheva ataingoza Genoa kwenye mchezo wake wa kwanza kama Kocha Mkuu dhidi ya Mwalimu wake wa zamani Jose Mourinho wa AS Roma siku ya Novemba 14 kwenye Uwanja wa Luigi Ferraris.


Wawili hao walishinda Kombe la Ligi na Kombe la FA msimu wa 2006/07 walipokuwa pamoja Stamford Bridge mpaka Roma ya Mourinho iko nafasi ya sita kwenye Serie A baada ya kushinda mara sita, kufungwa mara tano na kutoka sare moja hadi sasa. Giallorossi walishindwa kwa mabao 3-2 na Venezia siku ya Jumapili jambo ambalo liliwafanya wabaki nyuma ya vinara wa ligi Napoli.


Post a Comment

0 Comments