seebait header

MTOTO WA MIAKA 14 ALIVYOUWAWA KWA KUFUNGIWA SHOTI MAREKANI


Hauwezi kumnyima mtu haki yake bali unaweza kuicheleweshaGeorge Junius Stinney Jr. Mmarekani mwenye asili ya kiafrika, ndiye kijana mdogo mwenye umri wa miaka 14 aliehukumiwa kifo cha umeme kwenye kiti mnamo mwaka 1944 nyumbani kwao Alcolu, South Carolina, alihukumiwa kifo hicho baada ya kuonekana wamwisho kua na wasichana wawili wa kizungu Betty Benniker-11 na Merry Thames-8 waliokutwa wamekufa na chanzo cha kifo chao kutojulikana

Kesi hii ilitolewa ushahidi na askari polisi waliodai kwamba George amekiri kuhusika na mauaji hayo licha ya kutokuwepo maandishi yeyote toka kwa George yanayoonyesha kukiri kwa sakata hilo. Hata hivyo madaktari wa kizungu walioambatana na polisi wa kizungu ndio walienda kuifanyia miili postmortem (baada ya kifo)

Aidha kesi ilichukua siku moja tu, jopo la majaji wa kizungu lilitoa maamuzi moja kwa moja kutokana na kwamba watu weusi wakati huo hawakua na elimu ya kuwafanya wazingatiwe. Hukumu ya kesi iliamuru George Junius Stinney kuuwawa kwa kuketishwa katika kiti cha umeme

George aliwekewa mfano wa sufuria kichwani ili kumuongezea uzito kusaidia kiti kutoa umeme kwakua uzito wake haukutosha, umeme wa 2400V uliwashwa na kusitisha maisha ya kijana huyo huku kichwa chake kikifumuka vibaya mpaka kuonyesha sehemu ya fuvu lake.

Kundi la watu lilifanyia uchunguzi wa kesi yake ili kupata haki ya George. Ndipo mwaka 2013 familia yake ilifungua kesi ya madai, mnamo desemba 2014 hukumu yake ilibatilishwa  baada ya kua tayari ameshatendewa makosa, jaji wa mahakama hiyo alisema, George hakutendewa haki na haki zake za msingi zilikiukwa.

Post a Comment

0 Comments