seebait header

GOSPEL AUDIO/VIDEO: GOODLUCK GOZBERT – HAUWEZI KUSHINDANA | LYRICS


Kutoka kwenye albamu yake mpya na yenye mguso wa kipekee iitwayo ”Shukurani” muimbaji anayefanya vizuri katika kiwanda cha muziki wa Injili nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla Goodluck Gozbert ameachia wimbo uitwao Hauwezi kushindana ukiwa ni wimbo wa tatu kutoka kwenye albamu hiyo ambayo ina mkusanyiko wa nyimbo nane ikiwa katika mfumo wa Audio CD.
Goodluck Gozbert ni moja kati ya waimbaji mahiri wa kizazi kipya cha muziki wa Injili nchini Tanzania aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana kazi zake nzuri za muziki zikidhihirisha uwezo wake wa kuimba nyimbo zenye tungo nzuri za kumsifu Mungu na kuinua nafsi na mioyo ya watu na kufanikiwa kunyakua tuzo kadhaa ambazo kwa hakika zimempa mafanikio makubwa kimuziki.


Albamu ya Shukurani kwasasa inapatikana sokoni waweza kupata nakala yako kupitia wakala wa Max Malipo waliopo sehemu mbalimbali nchini Tanzania.
Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kusikiliza na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua. Barikiwa!









Post a Comment

0 Comments